• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 24, 2015

  MBIO ZA OLIMPIKI YA RIO 2016; UGANDA YAIFUMUA RWANDA 2-1 KIGALI

  MABAO ya Nahodha Farouk Miya na Muzamiru Mutyaba aliyetokea benchi yameipa Uganda ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Rwanda 2-1 Uwanja wa Amahoro mjini Kigali jana katika mchezo  wa kufuzu Fainali za vijana Afrika chini ya umri wa miaka 23.
  Miya alifunga bao la kwanza dakika ya tisa kwa shuti la mpira wa adhabu lililoupasua ukuta wa Rwanda.
  Refa Souleiman Ahmed Djamal aliwapa Uganda adhabu hiyo baada ya kipa wa Rwanda, Olivier Kwizera kuucheza mpira kwa mguu mmoja nje ya eneo la penalti. 
  Kipindi cha pili, wenyeji walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 59 kupita kwa kiungo kinda Dominique Savio Nshuti, kabla ya dakika 10 baadaye Muzamiru Mutyaba kuifungia Uganda bao la ushindi akitumia makosa ya kipa Kwizera kutoka langoni bila mahesabu.
  Timu hizo zitarudiana mjini Kampala, Uganda na mshindi wa jumla atamenyana na Misri katika mechi ya mwisho ya kufuzu kwa fainali za U-23 za Afrika ambazo zitafanyika Dakar, Senegal, kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 12. 
  Timu tatu za juu kutoka michuano hiyo ya Afrika zitakwenda Olimpiki ya Rio 2016 nchini Brazil.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBIO ZA OLIMPIKI YA RIO 2016; UGANDA YAIFUMUA RWANDA 2-1 KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top