• HABARI MPYA

  Thursday, May 28, 2015

  MSHINDI KWETU HOUSE YA AZAM TV KUONDOKA NA SH MILIONI 15

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHINDI wa shindano la Kwetu House la Azam TV, ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 15, imeelezwa. 
  Meneja Chaneli wa wa Azam TV, Stellah Adams amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Azam TV, makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, Dar es Salaam kwamba wanaona fahari kutangaza uzinduzuzi wa msimu wa pili wa Kwetu House. 
  “Kama inavyofahamika, Kwetu House ni kipindi chenye lengo la kuonyesha vipaji tofauti ambavyo ni kielelezo cha vipawa vingine alivyojaaliwa shabiki wa kweli,”amesema.
  Ameongeza kwamba shindano linahusu kuwaweka pamoja mashabiki mbalimbali katika jumba moja ili washindane na hatimaye kumpata shabiki wa kweli ambaye ataondoka na donge nono la Sh. Milioni 15.
  Meneja Chaneli wa Azam TV, Stellah Adams kulia akifafanua jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo


  Wakuu wa Azam TV katika mkutano na Waandishi wa Habari leo

  Kwa uopande wake, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington amesema kwamba msimu wa pili wa Kwetu House ambao kauli mbiu yake ni “Kwetu House, Kipaji zaidi ya soka”.
  “Kwa mara nyingine itawakusanya mashabiki wa kandanda wenye vipaji tofauti ili wawanie zawadi kubwa. Vipindi hivi vitakavyoandaliwa na Uhai Productions – chombo cha Azam Media kinachohusika na utayarishaji wa vipindi, vitarushwa katika chaneli mbili za Azam One na Azam Two,”amesema. 
  Amesema safari hii Kwetu House itahusisha washiriki 20 ambao watathibitisha ushabiki wao kwa klabu mbalimbali za soka za hapa Tanzania na zingine za kimataifa, kupitia shughuli mbalimbali, na pia wataweza kuonesha vipaji vyao. 
  “Msimu huu, Kwetu House inasaka zaidi shabiki inakwenda mbali Zaidi na kusaka shabiki wa kweli lakini pia mwenye kipaji.  Watakuwepo watu mashuhuri wanaofahamu vema maana ya kipaji Ili kusaidia kuwanoa! Shabiki huyu wa ukweli atalazimika kuwa na mvuto wa kipekee, awe mwelewa wa mchezo wa kandanda na awe tayari kufanya lolote la kumwezesha kuibuka mshindi,”amesema. 
  Ameongeza kwamba msimu wa pili wa Kwetu House utaanza Juni hadi Septemba 2015 na utahusisha pia washiriki wa kike na kutakuwa na vipindi vya kila siku na pia kipindi cha juma ambacho kitahusisha pia watazamaji kuwasiliana na washiriki kupitia mitandao ya kijamii.
  “Ili kushirikikisha mashabiki wengi kutoka  nchi, msimu wa pili wa Kwetu House utahusisha washiriki kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Unguja, jambo ambalo lita endesha mchujo utakao zaa washiriki 20 wa mwisho,”amesema. 
  Fomu za usajili zitapatikana kuanzia June Mosi 2015 katika ofisi zote za mawakala zilizotapaa nchi nzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSHINDI KWETU HOUSE YA AZAM TV KUONDOKA NA SH MILIONI 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top