• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 24, 2015

  TFF YATISHIA KUZIFUTA LIGI KUU SIMBA NA YANGA, KISA…

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. 
  Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16. Simba na Yanga ni klabu kongwe katika Ligi Kuu, ambazo zinaweza kukumbwa na adhabu hiyo zisipotekeleza agizo hilo. 
  Wachezaji wa klabu kongwe, SImba (jezi nyekundu) na Yanga SC (jezi za njano) wakisukumana katika moja ya mechi zao

  Katika hatua nyingine, kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YATISHIA KUZIFUTA LIGI KUU SIMBA NA YANGA, KISA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top