• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 21, 2015

  LIVERPOOL YAAMUA KUMPOTEZEA STERLING, BAADA YA MENENO YA 'NYODO' YA WAKALA WAKE

  KLABU ya Liverpool imefuta mpango wa kufanya mazungumzo na washauri wa Raheem Sterling yaliyotarajiwa kufanyika kesho, kufuatia wakala wake 'kusema mbovu'.
  Katika gazeti la London Evening Standard, Aidy Ward amesema Sterling hatasaini Mkataba mpya Liverpool hata apewe ofa ya mshahara wa Pauni 700, 000, 800,000 au 900,000 kwa wiki, hivyo kwa maana hiyo, Liverpool imeona hakuna sababu ya mazungumzo.
  Ward amekuwa akisistiza msimamo wake wiki yote hii, kabla ya kuweka wazi usiku wa Jumatatu kwamba kikao kilichoandaliwa na viongozi wa Liverpool kitaishia kwa Sterling kusema anataka kuondoka.
  Ward believes Sterling will leave the club
  Sterling was heckled at Liverpool's end of season awards on Tuesday night
  Sterling kulia akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka Liverpool na kushoto ni wakala wake, Ward 

  KUPANDA KWA MSHAHARA WA STERLING

  Pauni 400 kwa wiki - Wakati anacheza timu ya vijana ya QPR
  Pauni 2,000 kwa wiki - Wakati Sterling aliposaini Mkataba wake wa kwanza wa mchezaji wa kulipwa Liverpoool
  Pauni 35,000 kwa wiki - Kiasi anachopata Sterling katika Mkataba wake wa sasa Liverpool ambao umebakiza miaka miwili
  Pauni 100,000 kwa wiki - Kiasi ambacho Liverpool imeahidi kumpa katika Mkataba mpya anaokataa kusaini
  Liverpool imempa ofa ya mshahara wa Pauni 100,00 Sterling kwa wiki katika Mkataba mpya anaotakiwa kusaini ambao aliukataa February na mazungumzo baina ya pande hizo mbili yakapangwa kufanyika mwishoni mwa msimu.
  Mwanasoka huyo chipukizi wa kimataifa wa England alitarajiwa kuhudhiria na Ward.
  Sterling na Ward walitarajiwa kukutana na kocha Brendan Rodgers na Mtendaji Mkuu Ian Ayre mjini Liverpool kesho katika viwanja vya mazoezi vya Melwood.
  Lakini Liverpool imeamua haitafanya tena mkutano huo, baada ya Ward kuweka wazi msimamo wake.
  Ward anatarajia Manchester City au Chelsea kuwa klabu mpya ya Sterling, huku akikataa mpango wa kumpeleka kijana wake Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAAMUA KUMPOTEZEA STERLING, BAADA YA MENENO YA 'NYODO' YA WAKALA WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top