• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2015

    CHELSEA YANASA KINDA LA KIBRAZIL LENYE KIPAJI CHA HATARI, NI KIUNGO MBRAZIL NATHAN

    KINDA mwenye kijaji cha ajabu Mbrazil, Nathan ameadika kwenye akaunti yake ya Instagram kuthibitisha kuwasili kwake Ligi Kuu ya England akijiunga na mabingwa, Chelsea, kwa dau la Pauni Milioni 4.5.
    Kiungo huyo mshambuliaji mwenye mambo mengi, ambaye atatimiza miaka 19 Machi mwakani, alikuwa mjini London kwa mazungumzo mwezi Aprili na amefaulu vipimo vya afya katika viwanja vya mazoezi vya Chelsea, Cobham.
    Bado hakuna tamko rasmi la klabu, lakini Nathan ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram Jumatatu usiku, akithibitisha uhamisho huo.
    A photograph on Nathan's Instagram account appears to confirm his move to champions Chelsea
    Picha za Nathan katika akaunti yake ya Instagram akithibitisha kuhamia Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YANASA KINDA LA KIBRAZIL LENYE KIPAJI CHA HATARI, NI KIUNGO MBRAZIL NATHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top