• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 30, 2015

  YANGA YAIPIGA ‘BONGE LA BAO’ SIMBA, BUSUNGU ASAINI MIAKA MIWILI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeipa pigo lingine Simba SC, baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Malimi Busungu (pichani) wa Mgambo JKT ya Tanga.
  Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba wamemalizana na Busungu. 
  Dk Tiboroha amesema Busungu amesaini Mkataba wa miaka miwili leo kuhamia kikazi Yanga SC- maana yake Simba SC waliokuwa wanamuwania pia ‘imekula kwao’.
  “Huyu kati ya wachezaji ambao walipendekezwa na benchi la Ufundi. Tumefanikiwa kumalizana naye leo hii,”amesema Tiboroha.  
  BIN ZUBEIRY inafahamu Simba SC ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo, lakini wakashindwana dau.
  Malimi Busungu sasa anapatikana Jangwani, Dar es Salaam na atakuwa anavalia jezi za rangi ya kijani na njano

  Busungu amekuwa mchezaji tegemeo wa Mgambo JKT kwa misimu mitatu na wiki hii aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
  Busungu anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Yanga SC ndani ya wiki moja na ushei, baada ya awali timu hiyo kuwasajili winga kipa Benedictor Tinocco wa Kagera Sugar, beki Mwinyi Hajji Mngwali wa KMKM na mshambuliaji Deusi Kaseke kutoka Mbeya City. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAIPIGA ‘BONGE LA BAO’ SIMBA, BUSUNGU ASAINI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top