• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 29, 2015

  BLATTER ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI FIFA, WAZUNGU VICHWA CHINI!

  RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter amechaguliwa tena kuendelea kushika wadhifa huo katika uchaguzi Mkuu uliofanyika leo mjini Zurich, Uswisi.
  Blatter amepata kura 133 katika raundi ya kwanza na Prince Ali akapata kura 73. Kwa kuwa Blatter hakupata nusu ya kura zote (140), uchaguzi ulielekezwa katika raundi ya pili, lakini mpinzani wake Prince Ali akajitoa. 
  Maana yake, babu wa umri wa miaka 79, Blatter ataendelea kuongoza soka duniani kwa awamu ya tano.
  Blatter ameshinda uchaguzi huo kiume haswa, kwani alikuwa anapigwa vita kubwa na nchi za Ulaya chini ya Shirikisho lake, UEFA wakiongozwa na Uingereza.
  Kuelekea uchaguzi huu, kashfa nyingi ziliibuliwa ikiwemo ya rushwa ya Pauni Milioni 100, ambayo Wazungu waliishikia bango wakitaka Blatter aachie ngazi. Victory: Sepp Blatter (pictured) celebrates after his re-election as president of FIFA in Zurich on Friday night
  Ushindi: Sepp Blatter akisherehekea baada ya kushinda uchaguzi wa FIFA usiku huu mjini Zurich, Uswisi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BLATTER ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI FIFA, WAZUNGU VICHWA CHINI! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top