• HABARI MPYA

    Tuesday, May 19, 2015

    NYOTA MPYA MAN UNITED ABEBA KIATU CHA DHAHABU UHOLANZI

    MSHAMBULIAJI wa PSV, Memphis Depay amethibitishwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie baada ya mechi za mwisho za ligi hiyo Jumapili. 
    Kinda huyo wa umri wa miaka 21, ambaye amekubali kujiunga na Manchester United msimu ujao kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25, amefunga mabao 22 katika mechi 30 alizocheza, na kuwa mchezaji mdogo zaidi kutwaa tuzo hiyo tangu mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldo mwaka 1995.
    Depay amekuwa na mchango mkubwa kwa PSV kutwaa taji la ligi ya Uholanzi msimu huu, kikosi cha kocha Phillip Cocu kikiwazidi kwa pointi 17 Ajax walioshika nafasi ya pili. Walimalizia msimu kwa ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya ADO Den Haag.
    PSV forward Memphis Depay has been named the Eredivisie's top goalscorer for the 2014-15 season
    Mshambuliaji wa PSV, Memphis Depay ametwaa tuzo ya ufungaji bora Eredivisie msimu wa 2014-2015 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA MPYA MAN UNITED ABEBA KIATU CHA DHAHABU UHOLANZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top