• HABARI MPYA

    Thursday, May 28, 2015

    MANGO GARDEN NYEUPE WIKI HII, BURUDANI NI MOJA TU …YAMOTO BAND NA MASHAUZI LEO USIKU

    KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden Kinondoni unapitisha wikiendi bila burudani yoyote na badala yake onyesho la Yamoto Band na Mashauzi Classic leo usiku ndio show pekee wiki hii katika ukumbi huo. 
    Kesho Ijumaa  Malaika Band ambao hupiga hapo Mango kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini.
    Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.
    Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la nyama choma.
    Yamoto Band watakwea jukwaa la Mango Garden Kinondoni leo usiku (Alhamisi, 28) kuonyeshana kazi na wenyeji wao Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi.
    Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANGO GARDEN NYEUPE WIKI HII, BURUDANI NI MOJA TU …YAMOTO BAND NA MASHAUZI LEO USIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top