• HABARI MPYA

    Tuesday, May 19, 2015

    WEST BROM WAWATANDIKA MABINGWA CHELSEA 3-0 THE HAWTHORNS

    MABINGWA Chelsea wamefumuliwa mabao 3-0 na West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa The Hawthorns.
    Saido Berahino alifunga bao la kwanza kwa wenyeji dakika ya tisa, kabla ya kiungo wa The Blues, Cesc Fabregas kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28 kwa kuupiga mpira kwa Chris Brunt wakati refa amesimamisha mchezo.
    Berahino akafunga bao la pili dakika ya 47 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na John Terry.
    Chris Brunt akaongeza shangwe za mashabiki wa nyumbani baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 60. Mchezo huo haukuwa na umuhimu kwa timu yoyote, Chelsea ikiwa tayari bingwa West Brom imejihakikishia kubaki Ligi Kuu.
    Kikosi cha West Brom kilikuwa: Myhill, Dawson, McAuley, Olsson, Lescott, Brunt, Fletcher, Yacob, Morrison/Baird dk89, McManaman/Gardner dk54 na Berahino/Ideye dk79.
    Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Loftus-Cheek/Ake dk73, Matic, Remy/Brown dk79, Fabregas, Hazard na Diego Costa/Cuadrado dk64.
    The 21-year-old points to the skies after netting his 13th Premier League goal of an impressive season
    The 21-year-old points to the skies after netting his 13th Premier League goal of an impressive season PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WEST BROM WAWATANDIKA MABINGWA CHELSEA 3-0 THE HAWTHORNS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top