• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 24, 2015

  TIDO MHANDO WA AZAM TV ‘AULA’ TFF

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeteua Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Mhando (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Soka (FDF).
  Katika Kamati hiyo, Mhando atasaidiwa na Deogratius Lyatto atakayekuwa Makamu wake mwenyekiti na Wajumbe Ephraim Mafuru, Beatrice Singano, Joseph Kahama, Ayoub Chamshama wakati Henry Tandau atakuwa Katibu mtendaji wa mfuko huo.
  Uteuzi huo umefanyika katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF leo chini ya Rais wake, Jamal Malinzi.
  Aidha, kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, Kamati ya Utendaji kwa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIDO MHANDO WA AZAM TV ‘AULA’ TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top