• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 19, 2015

  ZIMBABWE, NAMIBIA ZOTE ZASHINDA COSAFA, SASA KUKUTANA KATIKA MECHI YA KIFO ALHAMISI

  Na Mahmoud Zubeiry, RUSTERNBURG
  TIMU za taifa za Zimbabwe na Namibia zitakutana katika mechi ya mwisho kali ya Kundi A Kombe la COSAFA Alhamisi kuwania nafasi ya kwenda Robo Fainali.
  Hiyo inafuatia timu zote kupata ushindi dhidi ya timu za visiwani katika mechi za Kundi A leo Uwanja wa Moruleng mjini hapa.
  Zimbabwe imeshinda 1-0 dhidi ya Shelisheli bao pekee la Chawaphiwa dakika ya 53, wakati Namibia imewafunga Mauritius 2-0, mabao ya Shilongo dakika ya nne na 66 kwa penalti.

  Hiyo inamaanisha Namibia watahitaji lazima kushinda Alhamisi, wakati Zimbabwe watagombea sare tu ili kuongoza Kundi A.
  Michuano hiyo itendelea kesho Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kwa mechi za Kundi B, waalikwa kutoka Afrika Mashariki, Tanzania wakimenyana na Madagascar, wakati Lesotho watamenyana na Swaziland.
  Tanzania ilifungwa 1-0 na Swaziland katika mchezo wa kwanza, wakati Madagascar ilishinda 2-1 dhidi ya Lesotho jana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZIMBABWE, NAMIBIA ZOTE ZASHINDA COSAFA, SASA KUKUTANA KATIKA MECHI YA KIFO ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top