• HABARI MPYA

    Sunday, May 10, 2015

    LIVERPOOL WAJIANDAA 'KUMPOSA' MKONGWE ANDREA PIRLO ALIYEWAFUNGA MIDOMO REAL MADRID

    KOCHA Brendan Rodgers atajaribu kumajili kiungo mkongwe wa Juventus, Andrea Pirlo amuhamishie Liverpool msimu ujao.
    Pirlo alikuwa kivutio wakati Juve ikiichapa mabao 2-1 Real Madrid Jumanne katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini baada ya mechi hiyo Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema ataondoka klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
    Pirlo ameweka wazi kwamba hana mpango wa kujiunga na timu nyingine yoyote ya Serie A na amegusia atakaribisha ofa kutoka timu za Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
    Andrea Pirlo pulled the strings for Juventus in their 2-1 Champions League victory over Real Madrid 
    Andrea Pirlo aliiongoza Juventus kuilaza 2-1 Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Turin 

    Lakini uamuzi wake huo umeziamsha klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England, hususan Liverpool wanaomtaka akazibe pengo la Nahodha wao, Steve Gerrard anayehamia LA Galaxy mwishoni mwa msimu.
    Licha ya umri wake mkubwa, Pirlo amedhihirisha tena katika mechi dhidi ya Real kwamba uwezo wake bado mkubwa katika kuiongoza timu, kutoa pasi maridadi katika eneo la kiungo.
    Pirlo anaweza kuondoka kwa ada ndogo tu ya uhamisho hata kama mchezaji huru, ambayo inaweza kuipa fursa Liverpool kumudu gharama binafsi za mchezaji huyo.
    Wekundu hao watatakiwa japo kutoa mara mbili ya ofa yao, Pauni Milioni 7 kama wanamtaka kiungo wa Inter Milan, Mateo Kovacic.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL WAJIANDAA 'KUMPOSA' MKONGWE ANDREA PIRLO ALIYEWAFUNGA MIDOMO REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top