WAKALA Jonathan Barnett wa mchezaji Gareth Bale amesema kijana wake anasota Real Madrid kwa sababu wachezaji wenzake hawampi pasi za kutosha.
Lakini Barnett amesema winga huyo wa kimataifa wa Wales hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo.
Lakini Barnett amesema winga huyo wa kimataifa wa Wales hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo.
Bale amejikuta katika msimu wa pili mgumu Hispania Jumanne tu iliyopita akitoka kucheza kwa kiwango cha chini Real ikifungwa na Juventus 2-1 na Jumamosi akashindwa kuisaidia timu yake hiyo ikilazimishwa sare ya 2-2 na Valencia katika La Liga.
Tayari ameanza kuzongwa na kuzomewa na mashabiki Uwanja wa Bernabeu, licha ya kwamba alifunga mabao katika fainali za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Mfalme msimu uliopita Rea ikitwaa mataji yote hayo.
Real ilivunja rekodi ya usajili wa 'bei mbaya' kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, lakini wameshindwa kupata walichokitarajia kutokana na mchezaji huyo kuandamwa na majeruhi.
"Real wanatakiwa kufanya kazi na Gareth na kumpasia mipira zaidi,"amesema wakala wa Bale, Jonathan Barnett.
"Mpe mipira zaidi na acha amuonyeshe kila mmoja uzuri wake. Atakuwa mchezaji bora Real Madrid wakati wachezaji wenzake watakapoanza kushirikiana naye na kumsaidia," amesema.


.png)
0 comments:
Post a Comment