STEVEN Gerrard amewaaga Liverpool kwa bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 ya mabingwa, Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Old Trafford.
Gerrard aliyeanza kuchezea akademi ya Liverpool mwaka 1987 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 1998, amefunga bao lake la 119 leo katika mechi 502 alizoichezea timu hiyo na sasa anahamia Marekani kumalizia soka yake.
Nahodha huyo wa Wekundu hao, alifunga bao hilo dakika ya 44- kufuatia Nahodha wa Chelsea, John Terry kuanza kuwafungia mabingwa hao dakika ya tano.
Liverpool walilazimika kujipanga mistari miwili kuwapa heshima yao wachezaji wa Chelsea waliopita katikati yao kabla ya mechi kufuatia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Kinda wa miaka 19, Ruben Loftus-Cheek alichezea kwa mara ya kwanza kikosi cha Jose Mourinho katika Ligi Kuu England.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Zouma/Cahill dk35, Terry, Luis, Mikel, Loftus-Cheek/Matic dk60, Willian, Fabregas, Hazard na Remy/Cuadrado dk84.
Liverpool; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Johnson, Henderson, Gerrard/Lucas dk79, Coutinho, Sterling, Lambert/Sinclair dk68, Lallana/Ibe dk71.
Gerrard alitolewa mwishoni mwa mchezo baada ya kuifungia bao la kusawazisha Liverpool Uwana wa Stamford Bridge leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment