• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2015

    AZAM FC YAWABORESHEA MIKATABA MAKINDA WAKE SABA, SASA WAANZA KUVUNA MATUNDA YA SOKA YAO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imeboresha mikataba ya wachezaji wake saba chipukizi iliyowapandisha kutoka akademi msimu uliopita na sasa wamepewa mikataba ya wachezaji rasmi wa kulipwa.
    Hao ni mabeki, Bryson Raphael, Ismail Gambo ‘Kussi’, Gardiel Michael, viungo Kevin Friday, Farid Malik Mussa, Mudathir Yahya na mshambuliaji Optatus Lupekenya.
    Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba klabu imeamua kuboresha mikataba ya makinda hao baada ya kuvutiwa na uwezo wao.
    Kevin Friday sasa 'anakunja' mshahara wa kueleweka Azam FC baada ya Mkataba wake kuboreshwa

    “Ni wachezaji ambao pamoja na kwamba ni wadogo, lakini wamekuwa na mchango mkubwa katika timu msimu huu na wametudhihirishia kiu yao,” amesema Kawemba.
    Kwa sababu hiyo, Kawemba amesema klabu imeamua kuwasaidia kutimiza ndoto zao za siku moja kuwa wachezaji wa kulipwa wa Azam FC, kwa kuboresha mikataba yao.
    Azam FC imeshindwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga SC, walibuka mabingwa wapya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAWABORESHEA MIKATABA MAKINDA WAKE SABA, SASA WAANZA KUVUNA MATUNDA YA SOKA YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top