• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2015

    CANNAVARO, KIEMBA, CHANONGO WATEMWA STARS, KIKOSI CHAPAA KESHO KWENDA ‘SAUZI’

    Nahodha Nadir Cannavaro ameachwa kikosi cha Taifa Stars kinachokwenda COSAFA kwa sababu ya majeruhi
    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameondolewa kwenye kikosi kinachoondoka kesho Jumatano kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la COSAFA.
    Cannavaro ameondolewa baada ya kupimwa afya jana na madaktari wa Taifa Stars na kugundulika bado majeruhi.
    Majeruhi wengine walioondolewa Taifa Stars ni Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo na Kelvin Friday. 
    Wachezaji hao watabaki nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON.
    Kiungo Amri Kiemba amepewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
    Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng  jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
    Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.
    Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.
    Kesho siku ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ni muda wa mapumziko, waandishi wa habari mnakaribishwa katika kambi ya timu ya Taifa iliyopo Tansoma Hotel kuweza kuongea na wachezaji, kocha mkuu na daktari wa timu kabla ya kuanza safari jioni.
    Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni makipa; Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Mwadini Ali (Azam), mabeki ni Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).
    Wengine ni viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar).
    Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco na Juma Luizio (Zeco United).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO, KIEMBA, CHANONGO WATEMWA STARS, KIKOSI CHAPAA KESHO KWENDA ‘SAUZI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top