Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIMBA SC itamuongezea Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kipa wake namba moja, Ivo Philips Mapunda baada ya kazi nzuri jana akiiongoza timu hiyo kushinda 1-0 dhidi ya mahasimu wa jadi,Yanga SC.
Ivo alidaka kwa umahiri mkubwa jana Simba SC ikiendeleza ubabe kwa mahasimu, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na baada ya mechi kocha Mserbia, Goran Kopunovic akampongeza mkongwe huyo kwa kazi nzuri ya kuokoa michomo ya hatari langoni hadi timu ikashinda.
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akasema kwamba watamuongezea Ivo Mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
“Tutamuongezwa Mkataba wa mwaka mmoja na nusu, kama utakumbuka aliingia kwetu kwa Mkataba wa mwaka na nusu pia, maana yake ataitumikia Simba SC kwa miaka mitatu,”amesema Hans Poppe.
Ivo alisajiliwa Simba SC Desemba mwaka juzi kutoka Gor Mahia ya Kenya, baada ya awali kuzitumikia Bandari ya Mombasa nchini humo, St George ya Ethiopia, African Lyon na Yanga SC za Dar es Salaam, Moro United ya Morogoro, Prisons na Tukuyu Stars za Mbeya.
Hadi sasa, katika mechi nne ambazo Ivo amedaka dhidi ya Simba SC imeshinda tatu na sare moja. Mechi mbili za Nani Mtani Jembe Simba SC ilishinda 3-1 na 2-0 wakati za Ligi Kuu msimu uliopita zilitoka sare ya 1-1 kabla ya jana Wekundu wa Msimbazi kushinda 1-0.

![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia amesema Ivo ataongezewa Mkataba wa mwaka na nusu |
![]() |
| Ivo Mapunda amekuwa na maisha mazuri Simba SC tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia mwaka juzi |
“Tutamuongezwa Mkataba wa mwaka mmoja na nusu, kama utakumbuka aliingia kwetu kwa Mkataba wa mwaka na nusu pia, maana yake ataitumikia Simba SC kwa miaka mitatu,”amesema Hans Poppe.
Ivo alisajiliwa Simba SC Desemba mwaka juzi kutoka Gor Mahia ya Kenya, baada ya awali kuzitumikia Bandari ya Mombasa nchini humo, St George ya Ethiopia, African Lyon na Yanga SC za Dar es Salaam, Moro United ya Morogoro, Prisons na Tukuyu Stars za Mbeya.
Hadi sasa, katika mechi nne ambazo Ivo amedaka dhidi ya Simba SC imeshinda tatu na sare moja. Mechi mbili za Nani Mtani Jembe Simba SC ilishinda 3-1 na 2-0 wakati za Ligi Kuu msimu uliopita zilitoka sare ya 1-1 kabla ya jana Wekundu wa Msimbazi kushinda 1-0.

.png)
0 comments:
Post a Comment