• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 22, 2015

  SIMBA SC YAZINDUKA, YAIKUNG’UTA RUVU 3-0 TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imezinduka kutoka kwenye kipigo cha 2-0 cha Mgambo Shooting wiki iliyopita, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kukiwa hakuna bao na Simba SC ndiyo waliotawala mchezo na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Ruvu.
  Simba ilipata bao lake la kwanza dakika ya 60, mfungaji Ibrahim Hajibu kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki wa Ruvu, Said Madega kumfanyia madhambi Awadh Juma.
  Simba SC wakishangilia ushindi wao Taifa leo
   
  Ibrahim Hajib akilitia misukosuko lango la Ruvu leo Taifa

  Dakika moja baadaye, Awadh Juma aliifungia Simba SC bao la pili baada ya kujipasia mwenyewe na kupiga shuti.
  Mshambuliaji Elias Maguri aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi aliipatia Simba SC bao la tatu dakika ya 75, akimalizia pasi nzuri ya Said Ndemla.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 20, ikiwa nyuma ya Azam FC pointi 36 za mechi 18 na Yanga SC pointi 37 za mechi 18 pia.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Abdi Banda/Awadhi Juma dk46, Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’, Emmanuel Okwi/ Elias Maguli dk69 na Ibrahim Hajibu.
  Ruvu Shooting; Abdallah Abdallah, Michael Pius, Said Madega, Hamisi Kasanga, Ernest Ernest, Ally Mkanga, Juma Hamisi/Juma Mdindi dk71, Kassim Badi, Yahya Tumbo, Juma Mpakala na Abdulrahim Abdulrahim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAZINDUKA, YAIKUNG’UTA RUVU 3-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top