• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 23, 2015

  MKENYA ‘ARUSHA TAULO’ COASTAL UNION, JULIO SASA NDIYE ‘ZE BIG BOSS’

  Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
  KOCHA Mkenya James Nandwa amejiuzulu Coastal Union kutokana na matokeo mabaya, na uongozi wa klabu hiyo umempandisha mzalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuwa kocha Mkuu. 
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Coastal Union, Oscar Assenga ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii mjini hapa kwamba, Nandwa ameandika mwenyewe barua ya kujiuzulu.
  “Ni kwamba kocha Nandwa kaamua kuwajibika mwenyewe, na sasa Julio anakuwa kocha Mkuu,”amesema.
  Aidha, Assenga amesema aliyekuwa kocha wa African Sports, pia ya Tanga, Joseph Lazaro atakuwa kocha Msaidizi.
  James nandwa kulia 'amerusha taulo' Coastal Union baada ya matokeo mabaya Ligi Kuu

  “Joseph Lazaro ni kocha wetu wa muda mrefu, tuliwaazima African Sports ili awasaidie kwa muda na sisi (Coastal) tulikuwa tunaendelea kumlipa mishahara,”amesema Assenga.
  Lazaro ameisaidia Sports kurejea Ligi Kuu baada ya kupelekwa huko na klabu yake, Coastal kuwasaidia akifanya kazi na Kassim Mwabuda. 
  Hatua ya Nandwa kujiuzulu inakuja baada ya Coastal kufungwa na Azam FC jana 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Jamhuri Kihwelo sasa ndiye kocha Mkuu wa Coastal Union 

  Nandwa alitua Coastal mapema msimu huu, akirithi mikoba ya Mkenya mwenzake, Yussuf Chippo ambaye alichukuliwa na timu ya taifa ya kwao, Harambee Stars kama kocha Msaidizi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKENYA ‘ARUSHA TAULO’ COASTAL UNION, JULIO SASA NDIYE ‘ZE BIG BOSS’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top