• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  NIYONZIMA KUPIGA TEKE MEZA YA REFA AKAMULIWA ‘JIWE TANO’

  KIUNGO Haruna Niyonzima wa Yanga amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 37(f) kwa kupiga teke meza ya   mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. 
  Haruna alitolewa kawa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC, waliobuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi Machi 24, Machi mwaka huu mjini Dar es salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Haruna Niyonzima kushoto amepogwa faini kwa kupiga teke meza ya refa wa akiba

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA KUPIGA TEKE MEZA YA REFA AKAMULIWA ‘JIWE TANO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top