HAJJI SUNDAY MANARA 'ZUNGU' ALIPOANZA KAZI RASMI SIMBA SC LEO
Katibu wa Simba SC, Stephen Ally (kushoto) leo amemtambulisha rasmi Msemaji mpya wa klabu hiyo, Hajji Sunday Manara 'Zungu' (kulia) katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam. Hajji aliteuliwa wiki iliyopita kuwa Msemaji wa klabu hiyo. Hajji ni mtoto wa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Sunday Manara 'Computer' aliyewika klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment