• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 22, 2015

  SHETANI LACHINJA JOGOO ANFIELD, MATA APIGA ZOTE MBILI MAN UNITED IKIILAZA LIVERPOOL 2-1

  MANCHESTER United wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu, Liverpool jioni ya leo Uwanja wa Anfiled katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Kiungo Juan Mata aliifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 14, kabla ya Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kutolewa kwa kadi nyekundu kufutia kumchezea rafu Ander Herrera.
  Mkongwe huyo ambaye amekwishaweka wazi ataondoka Anfield mwishoni mwa msimu, alitolewa sekunde 40 tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Adam Lallana mwanzoni mwa kipindi cha pili.
  Mata akawafungia Mashetani Wekundu bao la pili dakika ya 59 akimalizia pasi nzuri ya winga Angel di Maria, kabla ya Daniel Sturridge kuifungia bao la kufutia machozi Liverpool dakika ya 69.
  Nahodha wa United, Wayne Rooney alikosa penalti dakika za lala salama, baada ya Daley Blind kuchezewa rafu kwenye boksi.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Sterling, Henderson, Allen, Moreno/Balotelli dk66, Lallana/Gerrard dk45, Coutinho na Sturridge.
  Manchester United; De Gea; Valencia, Jones, Smalling, Blind/Rojo dk94, Carrick, Herrera/Falcao dk83, Fellaini, Mata, Young/Di Maria dk55 na Rooney.
  Juan Mata kicks a corner flag after putting his side in the lead during the first half of the Barclays Premier League encounter at Anfield 
  Juan Mata akishangilia kwenye kibendera baada ya kuifungia bao la kwanza Man United Uwanja wa Anfield 
  Nyota wa Manchester United, Mata akibinjuka kuifungia United bao la pili leo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3006357/Liverpool-1-2-Manchester-United-Juan-Mata-nets-double-open-five-point-lead-Brendan-Rodgers-side.html#ixzz3V88LjdK9 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHETANI LACHINJA JOGOO ANFIELD, MATA APIGA ZOTE MBILI MAN UNITED IKIILAZA LIVERPOOL 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top