• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 23, 2015

  BEACH SOCCER YAREJEA LEO BAADA YA 'KUSHUGHULIKIWA' NA MISRI

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) inarejea leo mchana saa 8:45, kwa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri ambapo jana ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.
  Rais Malinzi amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.

  Ili kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo mchezo huo unachezwa  Dar es salaam na Zanzibar.
  Katika mchezo wa jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum (1), Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
  Misri imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya Shelisheli, zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEACH SOCCER YAREJEA LEO BAADA YA 'KUSHUGHULIKIWA' NA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top