• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 31, 2015

  BANDA AMTWANGA ‘HADI DAMU’ HAJIBU MAZOEZINI SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES BSALAAM
  WACHEZAJI tegemeo wa Simba SC, kiungo Abdi Banda na mshambuliaji Ibrahim Hajibu jana walichapana makonde katika mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Banda ndiye aliyemvaa Hajibu na kuanza kumsukumia ‘mweda’ baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji mwenzake huyo kumchezea rafu mbaya.
  Hajibu alimpiga teke la tumboni Banda, ambaye kwa hasira akaamua kutumia mikono yake mirefu kumtandika ngumi mchezaji mwenzake huyo. Hajibu naye akaanza kujibu- ngumi zikapigwa kwa dakika chache, kabla ya wachezaji wenzao kuwatenganisha.
  Ibrahim Hajibu kushoto jana alipigana na Abdi Banda mazoezini Simba SC

  Waliowatenganisha wachezaji hao ni Jonas 
  Mkude, Awadh Juma, William Lucian ‘Gallas’, Emmanuel Okwi na wachezaji wengine.
  Baada ya ‘ndondi hizo’ zilizosababisha mazoezi ya jioni ya Simba SC yasimame kwa takriban nusu saa, Hajibu alionekana akitokwa damu mdomoni kutokana na ‘vitasa’ vya Banda, ambaye naye alikuwa analalamikia maumivu ya tumbo kutokana na teke la kikarateka la ‘Ibra Mabao’. 
  Baada ya wachezaji hao kutenganishwa, kocha Mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic aliwaita na kuzungumza nao kwa takriban dakika 15, kisha wakarejea kuendelea na mazoezi.
  Abdi Banda (katikati), jana amepigana na Ibrahim Hajibu mazoezini Simba SC 

  Kocha huyo Mserbia, Goran aligoma kuzungumzia suala hilo baada ya mazoezi akisema kwamba, halipo chini yake, bali ni viongozi ndiyo ndio wanaweza kulitolea tamko- bahati nzuri Katibu wa klabu, Ally Stephen alikuwepo, ingawa naye tayari kuzungumza, lakini ataliwasilisha kwa mabosi wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BANDA AMTWANGA ‘HADI DAMU’ HAJIBU MAZOEZINI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top