• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 29, 2015

  BRAZIL YAIKALISHA CHILE, YAICHAPA 1-0

  BRAZIL imeilaza bao 1-0 Chile katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Emirates, London England. 
  Bao hilo pekee limefungwa na Roberto Firmino dakika ya 72, baada ya kumzunguka kipa wa Chile, Claudio na kutumbukiza mpira nyavuni.
  Beki wa zamani wa Cardiff, Gary Medel alikuwa mwenye bahati kwa kutoonyeshwa kadi baada ya kumkita nyota wa Brazil, Neymar.
  Kikosi cha Brazil kilikuwa; Jefferson, Danilo, Thiago Silva, Miranda, Marcelo/Filipe Luis dk76, Souza/Elias dk60, Fernandinho, Douglas Costa/Willian dk62, Coutinho/Robinho dk60, Neymar na Luiz Adriano/Firmino dk60.
  Chile; Bravo, Medel, Jara, Albornoz, Isla, Millar/Fernandez dk74, Aranguiz, Mena/Gonazlez dk82, Vidal/Vargas dk80, Sanchez na Hernandez.
  Hoffenheim's Roberto Firmino (left) celebrates with team-mates Elias and Neymar having opened the scoring for Brazil against Chile
  Mchezaji wa Hoffenheim, Roberto Firmino (kushoto) akishangilia na wachezaji wenzake, Elias na Neymar baada ya kuifungia Brazil bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Chile leo.

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3016916/Brazil-1-0-Chile-Roberto-Firmino-settles-South-American-bragging-rights-Gary-Medel-escapes-nasty-stamp-Neymar.html#ixzz3VncMYn2W 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BRAZIL YAIKALISHA CHILE, YAICHAPA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top