• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  'TUTAKIMISI' KIFAA HIKI JUMAPILI MWANZA

  Kinara wa mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva hajachukuliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kitakachomenyana na Malawi Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kocha Mholanzi, Mart Nooij amemuacha mchezaji huyo kwa sababu yupo kwenye kikosi cha pili cha Stars, maarufu kama Taifa Stars Maboresho ambacho kitakuwa na mechi mwezi ujao. Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda. Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'TUTAKIMISI' KIFAA HIKI JUMAPILI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top