• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  SURE BOY WA AZAM FC KUPIGANA ATOZWA 500,000

  KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) na kufungiwa mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Adhabu kama hiyo imetolewa pia kwa mchezaji wa JKT Ruvu, Richard Maranya wa JKT Ruvu wote wakikabiliwa na kosa la kupigana uwanjani.
  Wawili hao waliweka kando mpira wa miguu na kuanza kutupiana masumbwi kwenye mechi namba 123 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam hadi wakatolewa nje kwa kadi nyekundu.
  Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam FC amepigwa faini kuwa kupigana na mchezaji wa JKT Ruvu

  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi Machi 24, Machi mwaka huu mjini Dar es salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SURE BOY WA AZAM FC KUPIGANA ATOZWA 500,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top