• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 24, 2015

  PETR CECH ABISHA HODI ARSENAL, REAL MADRID

  KIPA Petr Cech anatazamiwa kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya kuchoka kuwekwa benchi na Thibaut Courtois.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 raia wa Jamhuri ya Czech amepoteza namba mbele ya kipa kinda wa Ubelgiji, na Cech amedaka katika mechi nne tu za Lig Kuu ya England msimu huu, zaidi akitumia kwenye mechi za vikombe.
  Wakati akiukubali uamuzi huo wa kocha Mreno, Jose Mourinho, Cech, ambaye anaweza kuwa tegemeo kwa klabu kama Arsenal na Real Madrid, amesema sasa amechoka anataka kuondoka.
  Long-serving Blues goalkeeper Petr Cech is set to end his 11-year stay at Chelsea in the summer 
  Kipa wa muda mrefu wa The Blues, Petr Cech anatarajiwa kuhitimisha miaka yake 11 ya kuitumikia Chelsea mwishoni mwa msimu

  "Sijui klabu itakuwa na mawazo gani. Inaonekana kama inakwenda vizuri na mimi na Thibaut, kama wawili," amesema Cech. 
  "Lakini hiyo inaweza kufanya kazi kwa msimu mmoja tu. Sitaki hali kama hii tena,"amesema akiwa katika kambi ya timu yake ya taifa, Czech ambayo itacheza na Latvia katika mechi ya kufuzu Euro 2016 mjini Prague Jumamosi.
  Cech alijiunga na Chelsea mwaka 2004 na hadi sasa ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya FA, moja la Ligi ya Mabingwa, Europa League na matatu ya Kombe la Ligi na mara ya mwisho alidaka badala ya Courtios katika 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa Wembley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PETR CECH ABISHA HODI ARSENAL, REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top