• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  YAMOTO WASEPA NA DIMPOZ UMANGANI KUPIGA SHOO LA ‘KUFA MTU’

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  BENDI ya muziki wa kizazi kipya Yamoto Band na msanii wa kizazi kipya Ommy Dimpoz, kesho
  watafanya onesho maalum, kweye ukumbi wa Saol Gargen uliopo Mascat  Oman.
  Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuondoka nchini, Dimpoz, alisema kuwa wanaenda kwenye kufanya onesho moja  tu, ambalo litakuwa na kutumia vyombo moja kwa moja (Live).
  Dimpoz alisema hii ni mara ya pili kwa yeye kwenda Oman kufanya maonesho ya aina hiyo, lakini safari hii, alipoambiwa atafute bendi ya kwenda nayo, akaona Yamoto, ndiyo
  watakaoweza kukonga nyoo za mashabiki wao.
  Yamoto Band wakiwa Ommy Dimpoz Uwanja wa Ndege

  Alisema kuwa ana amini kwa upande wake atatoa burudani safi kwa kutumbuiza kutumia vyombo hata Yamoto wataacha gumzo katika nchini hiyo.
  "Nina amini tutaacha stori nchini Oman, maana tumejipanga kutoa burudani safi ya aina yake" alisema Dimpoz.
  Hata hivyo Dimpoz, alisema kuwa tayari tiketi za onesho hilo, zimeisha, hivyo wanaenda kufanya onesho hilo maalum ambalo limechukuliwa mpenzi mmoja wa muziki nchini humo.
  Kwa upande wa kiongozi wa bendi ya Yamoto, Asley Sadiq 'Dogo Aslay', alisema kuwa wameshukuru kupata nafasi hiyo,
  ambayo wana amini wataitumia vizuri.
  Alisema kuwa wamejipanga kutoa burudani ambayo itaacha maswali mengi, ambapo wapenzi
  wa bendi hiyo wajipange kupata burudani nzuri kutoka kwao.
  "Sisi kama kawaida yetu tutatoa burudani mwanzo mwisho, wakae vizuri kutupokea na kupata
  burudani ya aina yake"alisema Asley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAMOTO WASEPA NA DIMPOZ UMANGANI KUPIGA SHOO LA ‘KUFA MTU’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top