• HABARI MPYA

    Friday, March 27, 2015

    SIMBA SC, YANGA NA AZAM FC ZAKAMULIWA ‘MAHELA’ NA TFF KWA KUKIUKA KANUNI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    VINARA wa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wamepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(11) baada ya timu yake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano kwenye mchezo dhidi ya Simba SC.
    Mahasimu wao, Simba SC pia wamepigwa faini ya Sh. 300,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kukataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo namba 117 uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kilichofanyika Machi 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom  kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado.
    Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika ishirini.
    Klabu ya Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) baada ya timu yake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo namba 130 dhidi ya Young Africans uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
    Mechi namba 132 iliyozikutanisha Azam na Ndanda SC kwenye uwanja wa Chamazi, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) baada ya washabiki wake kuwamwagia maji na kuwarushia chupa za maji washabiki wa Azam.
    Aidha klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi namba 134 dhidi ya timu ya Mbeya City,  pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo.
    Kiongozi wa Stand United, Muhibu Kanu amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu baada ya kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumia lugha ya kuhamasisha vurugu kwa timu yake na kupinga uamuzi wa refarii.
    Katika mchezo namba 135 uliochezwa jijini Tanga na kuwakutanisha wenyeji Mgambo Shooting dhidi ya Yanga SC, Yanga SC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuvamia uwanja baada ya mechi namba 135 dhidi ya Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC, YANGA NA AZAM FC ZAKAMULIWA ‘MAHELA’ NA TFF KWA KUKIUKA KANUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top