• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 23, 2015

  SUAREZ ‘AWAMALIZA’ REAL MADRID, BARCA YAILAZA REAL MADRID 2-1 CAMP NOU

  BARCELONA imepig hatua moja mbele katika mbio za ubingwa wa Hispania, baada ya kuilaza Real Madrid mabao 2-1 katika mchezo wa La Liga usiku huu Uwanja wa Camp Nou.
  Ushindi huo wa El Clasico unaifanya sasa Barcelona iizidi kwa pointi nne Real kileleni mwa La Liga zikiwa zimebaki mechi 10.
  Jeremy Mathieu aliifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 19 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Lionel Messi kwa kumtungua kipa Iker Casillas.
  Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo akaisawazishia Real Madrid dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez kuifungia Barca bao la ushindi dakika ya 56.
  Kikosi cha Luis Enrique, Barca sasa kinatimiza pointi 68 baada ya kucheza mechi 28, wakati Real inabaki na pointi zake 64.
  Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Claudio Bravo, Gerard Pique, Javuer Mascherano, Jordi Alba, Dani Alves, Jeremy Mathieu, Ivan Rakitic/Sergio Bosquets dk76, Andres Iniesta/Xavi dk80, Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar/Rafinha dk 85.  
  Real Madrid; Iker Casillas, Pepe/Raphael Varane dk73, Sergio Ramos, Marcelo, Daniel Carvajal, Toni Kroos, Gareth Bale, Luka Modric/Lucas Silva dk88, Isco/Jese dk80, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
  Luis Suarez amefunga bao lake la kwanza katika El Clasico usiku huu Barcelona ikiilaza Real Madrid 2-1

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3006879/Barcelona-2-1-Real-Madrid-Luis-Suarez-scores-El-Clasico-winner-send-Catalans-four-points-clear-La-Liga-title-race-Jeremy-Mathieu-Cristiano-Ronaldo-goals-half.html#ixzz3V9hbrgWh 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUAREZ ‘AWAMALIZA’ REAL MADRID, BARCA YAILAZA REAL MADRID 2-1 CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top