• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 31, 2015

  LIGI DARAJA LA NNE YASHIKA KASI MWANZA

  Na Philipo Chimi, MWANZA
  LIGI ya Daraja la Nne Tanzania Bara msimu 2015 leo imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali mjini Mwanza, ambapo katika wilaya ya Nyamagana, timu ya Black Stars imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Talented FC mchezo ulio pigwa Uwanja wa Nyegezi jeshini, Mwanza.
  Katika mchezo huo, Talented FC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao mapema dakika ya nane kipindi cha kwanza kupitia kwa Nahodha wao, Everest Renatus, kabla ya Ephafra George kusawazisha dakika mbili baadaye.

  Katika kituo cha Butimba, timu ya Mwanza Terminal imeichakaza Opec international kwa mabao 5-2.
  Leo ligi hiyo itaendelea kwa kuzikutanisha timu za Liberty Shooting na Sankato FC katika kituo cha Nyegezi jeshini, wakati Butimba Biashara FC itaumana na Kilimo FC. Ligi hiyo inashirikisha timu 21 kutoka katika Wilaya ya Nyamagana mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI DARAJA LA NNE YASHIKA KASI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top