• HABARI MPYA

    Saturday, March 28, 2015

    MCHEZAJI SIMBA SC AHAMIA ‘BUSHI’

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZAJI wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”, Dua Said na muingizaji wa Bongo Movie, Lumole Matovola “Big” na Mwenyekiti wa Wasanii Tanzania  (SHIWATA), Cassim Taalib ni miongoni mwa wasanii 48 walioamua kwenda kuanza maisha ya kijijini.
    Wakizungumza katika mkutano wa bodi ya SHIWATA jana, wasanii hao walisema meamua kuungana na wasanii wengine wanaokwenda kuanza maisha mapya katika kijiji cha Wasanii, Mwanzega Mkuranga ambapo watapatiwa mashamba ya kulima bustani na mazao ya muda mfupi.
    Dua Said alisema amevutika na kujiji hicho na amekuwa mmoja wa wachezaji wa zamani kuanza maisha ya kijiji cgha wasanii ambayo alisema ni mazuri yenye manufaa kulinganisha na maisha ya mjini.
    Kwa muda mrefu Duwa Said amekuwa akiishi Kigogo, Dar es Salaam
    Duwa Said kushoto akiichezea Simba Veterani dhidi ya Yanga SC

    “Nimefika kijijini Mwanzega na mimi nimejengewa nyumba yangu na SHIWATA, pia nimerekodi filamu ambayo mtaiona katika luninga ni maisha mazuri ya kijijini  ambayo huwezi kufananisha na mjini” alisema Big.
    Mwenyekiti wa SHIWATA, Taalib alisema kati ya wanachama 8,000 ambao wamepanga kuhamia Mkuranga kwa ajili ya kilimo na ufugaji watashiriki katika sherehe za kutimiza miaka kumi kutoka ianzishwe na jumla ya nyumba 134 zimejengwa.
    Alisema mtandao huo unasikitishwa na taarifa ambazo siyo za kweli kuwa ndani ya mtandao huo kuna utapeli na kuongeza kuwa wanataarifu wanachama wo wote kwamba mpango huo ni wa kweli, uhakika na uwazi  hakuna mwanachama hata mmoja atakayepoteza haki yake kwa kujiunga na SHIWATA.
    Alisema Wanachama waliojiunga na SHIWATA kutoka mwaka 2004 na kufanikiwa kulipa sh. 10,000 za kujiunga na kijiji cha Mwanzega kupitia mtandao huo na kupatiwa hati wanatakiwa kufika ofisini Ilala Bungoni na nyaraka zao zote ili wapelekwe kijijini kukabidhiwa maeneo yao.
    Alisema pia wanachama wote waliochangia ujenzi ya nyumba zao kwa kiasi chochote cha fedha kupitia benki wanatakiwa kufika ofisini na nyaraka zao zote ili nao wakakabidhiwe maeneo yao kwa kadri walivyochangia.
    Alisema waliochangia katika mgawo wa mashamba katika shamba la Ngarambe na hatajakabidhiwa mashamba yao wanatakiwa wafike ofisini na nyaraka zao ili wakakabidhiwe.
    Alisema kijiji ambacho wanaamini kitakuwa kivutio kwa watalii nchini kitapewa jina la Tallywood na kutangazwa nchi mbalimbali duniani na kitakuwa maarufu kwa utengenezaji filamu ambazo zitauzwa ndani na nje ya Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI SIMBA SC AHAMIA ‘BUSHI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top