• HABARI MPYA

    Monday, March 30, 2015

    MECHI YA TAIFA STARS NA MALAWI YAINGIZA MILIONI 72

    Na Baraka Kizuguto, MWANZA
    MCHEZO wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika jana jumapili jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya wenyeji timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) umengiza jumla ya tsh 72.839,000 kutokana na idadi ya washabiki 15,762 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
    Mgawanyo wa mapato kwa mchezo hu ni VAT 18% sh. 11,111,103, gharama za tiketi sh. 3,203,700, gharama za mchezo (15%)sh. 8,778,639, Uwanja (15%) 8,778,639, CAF (10%) sh. 5,852,426 na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF (35%) sh. 35,114,560.
    Kikosi kilichoanza cha Stars jana mjini Mwanza

    Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini inatoa shukrani kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza  (MZFA) kwa ushirikiano wao katika kufanikisha maandalizi ya mchezo huo, waandishi na vyombo vya habari mbalimbali kwa sapoti waliyoitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
    Aidha TFF iinawashukru wapenzi, wadau na washabiki wa soka nchini, na hususani wa kanda ya ziwa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, kwani waliishangilia Taifa Stars tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho kwa ustaarabu wa hali juu.
    Katika mchezo huo Taifa Star ilitoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya The Flames, bao la wageni lilifungwa na Mecium Mhone kabla ya na Mbwana Samatta kuisawazishia Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA TAIFA STARS NA MALAWI YAINGIZA MILIONI 72 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top