• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  KOPONIVIC: SIMBA HII, OKWI ‘AKIWA UNGA’ TUMEKWISHA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amesema kwamba anahitaji mshambuliaji mwingine wa kiwango cha Mganda Emmanuel Okwi ili timu iwe vizuri.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY juzi, Kopunovic alisema kwamba kwa sasa Simba SC inamtegemea Okwi pekee, ambaye anapokuwa hayupo katika ubora wake, mambo yanakuwa magumu.
  Kopunovic amesema kwamba wachezaji wengine aliowategemea, wameshindwa kufanya vizuri kwa sasa na labda wengine wanahitaji muda.
  Kocha wa Simba, Goran Kopunovic anataka mshambuliaji mwingine wa kiwango cha Okwi

  “Kwa hawa wachezaji chipukizi wa hapa (Tanzania), wamekuwa hawachezi katika kiwango kile kile siku zote. Mtu anaweza akafanya vizuri katika mechi moja, halafu akashindwa kurudia katika mechi tatu,”amesema.
  Akimzungumzia mshambuliaji mwingine Mganda, Dan Sserunkuma aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia msimu huu, Kopunovic amesema huyo ni mchezaji mzuri, lakini kwa sasa ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa.
  “Sina wasiwasi kuhusu uwezo wa Dan, lakini katika wakati huu ambao timu inahitaji mabao, ameshindwa kufunga. Labda anahitaji muda. Lakini ukweli ni kwamba, nahitaji mtu wa aina ya Okwi katika timu,”amesema.
  Emmanuel Okwi ndiye mshambuliaji pekee tegemeo Simba SC kwa sasa

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOPONIVIC: SIMBA HII, OKWI ‘AKIWA UNGA’ TUMEKWISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top