• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  DANNY MRWANDA KUWANYIMA MKONO SIMBA KWAMTOKEA PUANI

  MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Dany Mrwanda  amepigwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(12) kwa kutopeana mikono na wachezaji wa Simba SC.
  Mrwanda anadaiwa kufanya hivyo katika pambano la watani wa jadi, SImba na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo timu yake ililala bao 1-0. 
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi Machi 24, Machi mwaka huu mjini Dar es salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Danny Mrwanda kushoto ametozwa faini kwa kugoma kuwapa mikono wachezaji wa Simba SC

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DANNY MRWANDA KUWANYIMA MKONO SIMBA KWAMTOKEA PUANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top