• HABARI MPYA

    Monday, March 30, 2015

    YAYA TOURE AFIKIRIA KUIVUA 'KIMOJA' JEZI YA IVORY COAST

    KIUNGO Yaya Toure amesema anafikiria kustaafu soka ya kimataifa baada ya kutimiza malengo yake.
    Toure aliiongoza nchi yake kama Nahodha kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika, hilo likiwa taji la kwanza kubwa baada ya zaidi ya miongo miwili na sasa anaweza kufuata nyayo za kaka yake, Kolo kuvua jezi Ivory Coast.
    Toure amesema atachukua siku kadhaa kuamua mustakabali wake, lakini amependekeza, kizazi kipya sasa lazima kipewe nafasi kikosi cha Tembo.
    Toure was in action during the draw with Equatorial Guinea in Abidjan, Ivory Coast, on Sunday 
    Toure aliichezea Ivory Coast ikitoa sare na Equatorial Guinea mjini Abidjan Jumapili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa

    "Mustakabali wangu?' aliuliza, alipoulizwa na BBC. "Inabidi usubiri. Sasa, malengo yangu yametimia. Tunapaswa kusubiri kwa siku kadhaa na kuona tutafanya nini,".
    "Kaka yangu amestaafu, na Copa (Barry, kipa wa muda mrefu wa Ivory Coast) naye pia. Muda wa nyota wanaochipukia utafika karibuni. Tunahitaji kuwaachia wao.
    Maneno haya ya Toure yanaweza kuwa habari njema kwa klabu yake, Manchseter City, ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kumkosa mchezaji huyo alipokuwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE AFIKIRIA KUIVUA 'KIMOJA' JEZI YA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top