• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 25, 2015

  DIEGO SIMEONE AANGUKA MKATABA MPYA ATLETICO MADRID HADI 2020

  KOCHA Diego Simeone amesaini Mkataba mpya wa kuendelea na kazi Atletico Madrid, ambao utamuweka katika klabu hiyo hadi mwaka 2020.
  Mabingwa hao watetezi wa Hispania walikwishaweka wazi mapema tu kwamba wanataka kuendelea na Muargentina huyo, ili awe ‘Sir Alex Ferguson wao’ na kutengeneza kasri mjini Madrid. 
  Na hatimaye juzi majadiliano yalikamilika na dada wa Simeone, ambaye pia ni wakala wake, Natalia juu ya Mkataba mpya ambao ni nyongeza ya miaka mitatu katika Mkataba wake wa sasa unaotarajiwa kumalizika mwaka 2017 ambao utamfanya alipwe mshahara wa Pauni Milioni 4.4 kwa mwaka. 
  Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone atadumu klabu hiyo hadi mwaka 2020
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIEGO SIMEONE AANGUKA MKATABA MPYA ATLETICO MADRID HADI 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top