• HABARI MPYA

  Wednesday, March 25, 2015

  PAN AFRICA FC NA CHANGANYIKENI FC KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA

  Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na timu za FFU na Zakhem kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao,kesho 20/03/2015 utapigwa mchezo mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi ya mikoa.
  Mchezo huo wa mtoano utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za Pan Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao.
  Pan African ni timu ya kihistoria Tanzania, ikiwa imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu 1982

  Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya kumpata mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa shirikisho la soka la Tanzania TFF.
  Aidha kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa Dar es salam tangu ilipoanza kutimua vumbi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAN AFRICA FC NA CHANGANYIKENI FC KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top