• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  TAMBWE KUMTOMASA SEHEMU ZA SIRI JUUKO, KESI YAPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU

  TUHUMA za mshambuliaji wa Yanga SC, Mrundi Amissi Tambwe kumshika sehemu zasiri beki wa Simba SC Murshid Juuko zimepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Tambwe anadaiwa ‘kumfinya korodani’ Mganda Juuko katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu hizo, Yanga SC ikilala 1-0.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi Machi 24, Machi mwaka huu mjini Dar es salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAMBWE KUMTOMASA SEHEMU ZA SIRI JUUKO, KESI YAPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top