• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 28, 2015

  ENGLAND YAUA 4-0 KUFUZU EURO, ROONEY ALIFUNGUA BIASHARA

  ENGLAND imeifumua mabao 4-0 Lithuania katika mchezo wa Kundi E Kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya usiku huu Uwanja wa Wembley, London, England.
  Nahodha Wayne Rooney alifunga bao la kwanza dakika ya sita hilo likiwa bao lake la 47 timu ya taifa, kabla ya Danny Welbeck kufunga la pili dakika ya 45.
  Raheem Sterling alimalizia krosi ya Rooney kufunga bal tatu dakika ya 58 kabla ya Harry 
  Kane kuhitimsha ushindi huo kwa bao la dakika ya 71 akiichezea England kwa mara ya kwanza.
  Ushindi huo, unaifanya England ifikishe pointi 15 baada ya mechi tano na kuendelea kujinafasi kileleni mwa kundi E, mbele ya Slovenia yenye pointi tisa sawa na Uswisi, wakati Lithuani ina pointi sita.
  Kikosi cha England kilikuwa; Hart, Clyne, Cahill, Jones, Baines, Henderson/Barkley dk71, Carrick, Delph, Sterling, Welbeck/Walcott dk76 na Rooney/Kane dk71. 
  Lithuania; Arlauskis, Freidgeimas, Zaliukas, Kijanskas, Andriuskevicius/Slavickas dk83, Chvedukas, Zulpa, Mikuckis/Stankevicius dk66, Mikoliunas/Kazlauskas dk88, Cernych na Matulevicius.
  Rooney and Welbeck embrace after the latter's goal gave England breathing space just before the break
  Rooney na Welbeck wakipongezana kwa kazi nzuri waliyoifanyia England 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3015343/England-4-0-Lithuania-Harry-Kane-scores-79-seconds-coming-Wayne-Rooney-Danny-Welbeck-Raheem-Sterling-seal-rout.html#ixzz3VdMkMoEt 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENGLAND YAUA 4-0 KUFUZU EURO, ROONEY ALIFUNGUA BIASHARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top