• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 30, 2015

  JEZI YA DI MARIA YAONGOZA KWA MAUZO ENGLAND, INAFUATIA YA SANCHEZ, DIEGO COSTA YA TATU

  HIZI ni habari njema ambazo zinaweza kumfariji Angel di Maria.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa ana msimu mgumu Manchester United uwanjani, lakini kiwango chake hakijaathiri umaarufu wake nje ya Uwanja kutokana na jezi kuongoza kwa mauzo katika Ligi Kuu ya England.
  Kwa mujibu wa muuzaji wa reja reja wa duka la Sports Direct, ambaye anauza jezi za timu za Arsenal, Aston Villa, Chelsea, Liverpool, United, Manchester City, Tottenham na Newcastle, jezi ya Di Maria inauliziwa na mtu mmoja karibu katika kila wanunua jezi tofauti 10. 
  Manchester United's record summer signing Angel di Maria tops the list of SportsDirect player shirt sales 
  Mchezaji ghali wa Manchester United, Angel di Maria anaongoza kwa kuuza jezi katika orodha ya SportsDirect
  Di Maria, Sanchez and Costa make up with top three with a combined share of 15.66 per cent
  Di Maria, Sanchez na Costa ndio wamo kwenye tatu bora wote kwa pamoja wakiwa na asilimia 15.66

  Jumla ya asilimia yake ni 9.59 ambayo inamfanya aongoze sokoni, akifuatiwa na nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez, mchezaji huyo wa Chile akiwa nafasi ya pili kwa asilimia 3.8.
  Di Maria amekuwa katika wakati mgumu uwanjani tangu asajiliwe kwa dau la Pauni Milioni 59.7 kutoka Real Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JEZI YA DI MARIA YAONGOZA KWA MAUZO ENGLAND, INAFUATIA YA SANCHEZ, DIEGO COSTA YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top