• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 30, 2015

  TENGA AISHUKURU TFF YA MALINZI KUMPA ‘SHAVU’ UCHAGUZI WA CAF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Chilla Tenga ameishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuunga mkono katika kugombea tena nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 7, mwaka huu mjini Cairo, Misri. 
  Tenga amesema hayo katika mkutano wa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kuzungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.
  Mwenyekiti wa CECAFA, Tenga kulia na Rais wa TFF, Malinzi kushoto.

  Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Tenga amezungumzia pia msimamo wa bara la Afrika uliowekwa katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mwaka jana jijini Sao Paulo, Brazil kuwa wanachama wote wa CAF watamuunga mkono Rais wa sasa wa FIFA anayetetea nafasi yake katika uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu jijini Zurich, Uswisi.
  Vilevile Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika Desemba 2014 jijini Nairobi, Kenya ulipitisha azimio la kumuunga mkono Joseph Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA.
  Katika mkutano huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa tamko rasmi kuwa kwa niaba ya TFF atampigia kura Joseph Sepp Blatter.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TENGA AISHUKURU TFF YA MALINZI KUMPA ‘SHAVU’ UCHAGUZI WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top