• HABARI MPYA

    Monday, March 09, 2015

    SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL 436

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MCHEZO namba 117 uliowakutanisha Simba na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana umeingiza Sh. 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
    Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.
    Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

    Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL 436 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top