• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 24, 2015

  MALAWI WAJA ALJHAMISI NA KAMWENDO WA TP MAZEMBE KUWAVAA STARS

  Joseph Kamwendo anakuja na Malawi
  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM 
  MSAFARA wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.
  Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
  Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).
  Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALAWI WAJA ALJHAMISI NA KAMWENDO WA TP MAZEMBE KUWAVAA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top