• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  MUSTAKABALI WA AMRI KIEMBA AZAM FC TATA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Amri Ramadhani Kiemba ana nafasi finyu ya kusajiliwa moja kwa moja kwa Azam FC anakocheza kwa mkopo kutoka Simba SC, kutokana na kushindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.
  Kiemba alitolewa kwa mkopo ‘kiroho safi’ kabisa na Simba SC Desemba mwaka akamalizie Mkataba wake unaofikia tamati mwishoni mwa msimu, lakini hadi sasa hajaweza kuwa na namba katika kikosi cha kwanza.
  Kiemba hakuweza kumshawishi kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyefukuzwa mwezi uliopita na ameshindwa pia kumvutia kocha wa sasa, Mganda George ‘Best’ Nsimbe.
  Amri Kiemba ameshindwa kuwashawishi makocha Azam FC kumpa nafasi kikosi cha kwanza

  Kiemba amekuwa akiingizwa dakika za mwishoni kabisa na hadi sasa ameingia mara 15 bila kufunga bao na mara nyingi zaidi amekuwa hatumiki kabisa.
  Wazi hiyo inamuweka pagumu kuweza kupewa Mkataba na mabingwa hao wa Tanzania Bara. Sasa, rasta huyo anakabiliwa na changamoto ya kumvutia kocha Nsimbe katika mechi zilizobaki kuelekea mwisho wa msimu, ili apewe nafasi zaidi. 
  Lakini bado watu wanaamini Kiemba ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuja kuisaidia Azam FC na kushindwa kung’ara kwake kutokana na kuopewa nafasi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MUSTAKABALI WA AMRI KIEMBA AZAM FC TATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top