• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  KITAULO CHA IVO SASA ACHUNGE SANA, VODACOM WAMPONZA

  KIPA wa Simba SC, Ivo Mapunda amepewa onyo kwa kufunika tangazo la mdhamini wa Ligi Kuu, Kampuni ya Vodacom kwa kutumia taulo lake wakati wa mechi dhidi ya Yanga SC.
  Aidha, Ivo ameambiwa atachukuliwa hatua kali za kinidhamu iwapo atarudia kufanya tukio la aina hiyo.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi Machi 24, Machi mwaka huu mjini Dar es salaam kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KITAULO CHA IVO SASA ACHUNGE SANA, VODACOM WAMPONZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top