• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2015

  KIINGILIO STARS NA MALAWI BUKU TANO

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetaja viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.
  Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa kuwakabili the Flames.

  Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba, ikiwa na kikosi  kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
  Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.
  Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.
  Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO STARS NA MALAWI BUKU TANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top