Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI wawili wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, mabeki Fatuma Khatib anayecheza kulia na Ziada Ramadhani wa kushoto, jana hawakufanya mazoezi na kikosi cha timu ya taifa, Twiga Stars kwa sababu ya maumivu.
Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ambaye anawaandaa wachezaji wake kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Zambia Machi 22, mwaka huu amesema kwamba wachezaji hao waliumia juzi.
Kaijage amesema wachezaji hao hawakufanya mazoezi jana wakiugulia maumivu, lakini anatarajia mapema wiki ijayo watakuwa fiti kwa kuwa wanaendelea vizuri na matibabu.
Kocha Kaijage ambaye alianza kambi yake mwishoni mwa mwezi uliopita anatarajiwa kuwa na mchezo mmoja wa kujipima nguvu katikati ya mwezi.
Twiga Stars ambayo imeweka kambi katika Hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Mbali na majeruhi hao wawili, wachezaji wengine walioitwa kikosini ni Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia Mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamisi Omar, Fadhila Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbas, Stumai Abdallah, Zuwena Aziz, Irene Joseph, Dawa Haji Vuai, Belina Julius na Amina Ramadhani.

![]() |
| Wachezaji wa Twiga Stars mazoezini jana Uwanja wa Karume, Dar es Salaam |
![]() |
| Nahodha wa Twiga Stars, Sofia Mwasikili akipoza 'koo' kwa maji ya Uhai baada ya mazoezi mazito jana |
![]() |
| Majeruhi Fatuma Khatib kushoto na Ziada Ramadhani wakiwa nje jana wakati wenzao wanaendelea na mazoezi jana Karume |
Kocha Kaijage ambaye alianza kambi yake mwishoni mwa mwezi uliopita anatarajiwa kuwa na mchezo mmoja wa kujipima nguvu katikati ya mwezi.
Twiga Stars ambayo imeweka kambi katika Hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Mbali na majeruhi hao wawili, wachezaji wengine walioitwa kikosini ni Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia Mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamisi Omar, Fadhila Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbas, Stumai Abdallah, Zuwena Aziz, Irene Joseph, Dawa Haji Vuai, Belina Julius na Amina Ramadhani.

.png)
0 comments:
Post a Comment